Tanzania
ni miongoni mwa nchi barani Afrika zinazoongoza kwa wagonjwa wenye
matatizo ya Moyo kufuatia idadi kubwa ya wananchi kubadili mifumo ya
maisha ikiwemo kutokufanya mazoezi na kupelekea kuwa na shinikizo la
damu.
Hayo yamebainisha jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano
uliowakutanisha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka nchi
mbalimbali barani Afrika ambapo mganga mkuu wa serikali nchini Tanzania
amesema jitihada za serikali hazitazaa matunda kama watanzania
hawatakuwa tayari kuzuia tatizo badala ya kutibu tatizo.
Rais wa
chama cha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini Docta Robert
Mvungi amsema mkutano huo unalenga kuchambua matatizo yanayopelekea
magonjwa hayo yanayogharimu maisha ya watu ili kuona namna ya kutoa
elimu na hatimae kupunguza magonjwa hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete amesema licha ya taasis hiyo kuendelea
kupunguza kwa asilimia kubwa wagonjwa kwenda kutibiwa nje bado tatizo
hilo kwa Tanzania limeendelea kuwa kubwa na kubaini ni vyema watanzania
wakaweka mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara ili kugundulika mapema
na kuweza kutibiwa.
Home
Afya
Slider
Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi barani Afrika zinazoongoza kwa Magonjwa ya Moyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment