Ndugu Waandishi wa Habari,
Hadi kufikia tarehe 18/04/2016 Mkoa wa Iringa
umefanya zoezi la uhakiki wa watumishi kwa awamu mbili awamu ya kwanza, uhakiki
ulifanyika kuanzia tarehe 16/03/2016 na kukamilika tarehe 26/03/2016 ambapo jumla
ya watumishi 15walibainika kuwa ni watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa ambao
waliisababishia Serikali hasara ya Shilingi 81,921,725.08.
Katika uhakiki wa awali Halmashauri ya Wilaya ya
Kilolo haikuwahakiki watumishi 159 kutokana na kuwa masomoni. Halmashauri hiyo
imekamilisha uhakiki huo ambapo imebainika watumishi wawili (2) ni watumishi
hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuhakikisha Mkoa unaondokana kabisa na tatizo la
watumishi hewa, niliwaelekeza Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na
Wakurugenzi wa Halmashauri kufanya zoezi hilo awamu ya pili.
Nimepokea
taarifa kutoka kwa Wakuu wa Wilaya inayoonesha kuwapo kwa watumishi hewa kumi
na mbili (12) hadi kufikia tarehe 18/04/2016. Watumishi hao wameisababishia
Serikali hasara ya shilingi 155,205,681/=
Uhakiki uliofanywa na Mkuu wa Wilaya katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umebainisha kuwapo kwa watumishi tisa (9) ambao ni watoro na mtumishi mmoja ambaye aliomba likizo bila malipo na kwenda kufundisha mahala pengine lakini akaendelea kulipwa mpaka kufikisha kiasi cha Tsh. 25, 831,000/= lakini baada ya kufanya ufuatiliaji amerejesha kiasi cha Tsh. 18,604,679/= Mtumishu huyu ni mwalimu anaitwa Dinner J. Kissamo alikuwa mwalimu Manispaa ya Iringa.
Aidha, Uhakiki pia ilibaini mwalimu mmoja (Ifunda) alikuwa na Check Na. 2 na zote alikuwa analipwa na halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika.
Mtumishi Mwingine ni Khalid M. Meza Afisa kilimo Kilolo ni mtoro wa muda mrefu mkurugenzi tayari ameshamfungulia mashtaka. Hii ni mifano tu ya watumishi hewa.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Ili kuendelea kujiridhisha na kuondolewa kabisa watumishi hewa katika Mkoa wa Iringa, nimechukua hatua zifuatazo;1. Nimewaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha kuwa, zoezi la uhakiki watumishi linakuwa endelevu na hatua zinachukuliwa ili kuwaondoa watumishi hewa wote
0 comments:
Post a Comment