Image
Image

Amnesty:Watoto wadogo wanaoshukiwa kuwa Boko Haram wameaga dunia wakiwa kizuizini.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema makumi ya watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram wakiwemo watoto wadogo wameaga dunia wakiwa kizuizini katika korokoro ya kijeshi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka huu pekee.
Ripoti mpya ya Amnesty International imesema watu 150 wamepoteza maisha katika kituo cha kijeshi cha Giwa katika mji wa Maiduguri chini ya mazingira magumu.
Netsanet Belay, Mkurugenzi wa Utafiti wa Amnesty International barani Afika amesema watoto saba na wengine wachanga wanne ni miongoni mwa washukiwa wa kundi la Boko Haram walioaga dunia katika kituo hicho kutokana na magonjwa, njaa, kuishiwa na maji mwilini na makovu ya risasi.
Amesema kuwa kubainika kuwa watoto wadogo ni miongoni mwa waliopoteza maisha katika kituo hicho cha kijeshi chini ya mazingira ya kuogofya ni jambo la kutisha na kutamausha.
Ripoti mpya ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu imebainisha kuwa, zaidi ya watu 1,200 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram wanazuiliwa katika kituo cha kijeshi cha Gewa mjini Maiduguri; na kwamba mmoja kati ya 10 miongoni mwao ni mtoto mdogo.
Kadhalika ripoti hiyo imetoa wito wa kufungwa kwa kambi hiyo ya mateso na washukiwa waachiwe huru mara moja au wahamishiwe katika jela za kiraia na wasaidiwe kupata mawakili.
Mwaka jana, Amnesty ilisema zaidi ya watu 7000 wamepoteza maisha chini ya mazingira magumu na ya kutatanisha katika kambi hiyo ya kijeshi tokea mwaka 2011.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment