Timu ya Manchester City huenda
ikapoteza nafasi ya kutinga Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa majirani zao
Manchester United baada ya Arsenal kupambana kiume na kulazimisha
sare ya mabao 2-2 katika dimba la Etihad Stadium.
Magoli yaliyofungwa na Sergio Aguero
na Kevin de Bruyne yaliipa Manchester City fursa ya kuongoza mara
mbili katika mchezo wa nyumbani wa kumuaga kocha wao Manuel
Pellgrini, anayeondoka baada ya msimu kumalizika.
Hata hivyo magoli ya Olivier Giroud
na Alexis Sanchez yalitosha kuonyesha uwezekano wa kocha mpya wa
Manchester City huenda akaanzia katika Ligi ya Uropa, na si Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Kevin de Bruyne akishangilia goli alilofunga
Sergio Aguero akijipinda na kuachia shuti lililojaa wavuni
0 comments:
Post a Comment