Mgodi
wa dhahabu wa Bulyanhulu na Taasisi ya Benjamin Mkapa zimekubaliana
kushirikiana katika kutekeleza mradi unaolenga kuboresha huduma ya afya
ya mama na mtoto katika wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga.
Akizungumzia
katika hafla ya kutia saini mkataba wa makubaliano hayo, Meneja Mkuu wa
mgodi wa dhahabu Bulyahnhulu Graham Crew amesema mgodi wake kupitia
mfuko wa maendeleo wa Acacia utatoa shilingi milioni 440 kugharamia
mradi huo.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa
Dkt.Ellen Senkoro amesema mradi huo wa miaka miwili utatekelezwa katika
kituo cha afya cha Bugarama na zahanati ya Kakola katika Halmashauri ya
wilaya ya Msalala.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment