Ameyasema hayo muda mfupi mara baada ya kufika katika kituo kikuu cha mabasi ya mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam kuona namna kazi inavyofanyika katika utoaji wa huduma za usafiri kwa wananchi wanaotumia mabasi hayo katika kusafiria kutoka eneo hilo Mpaka Posta.
Amesema kuwa kwa wafanya biashara wanaofanya shughuli zao hasa wale wanauza Samaki nivema sasa wakaweka kwenye ndoo ama kwenye mifuko migumu ili kusudi wapandapo ndani ya gari hizo harufu isichafue hali ya hewa kwani hata hivyo wanataka magari hayo yawe yanafungwa vioo nakuwashwa AC,kwani lengo hilo nikutaka kila mwananchi afurahie usafiri huo.
Majaliwa amesema kuwa kutokana na mfumo wa ukataji tiketi licha yakuwa umekuwa ukilalamikiwa lakini kama serikali wanahakikisha wanaboresha matumizi ya ukataji tiketi hizo ili kuepusha tatizo hilo lawatu kufanya udanganyifu wa tiketi moja kupanda mara mbili kwenye gari hizo za mwendo wa Haraka, ili kila mmoja awe na tiketi rasmi na sio iliyokwisha muda wake.
Hata hivyo Waziri Mkuu Majaliwa aliongozana sambamba na viongozi wengine wa mradi huo wa Dart,Pamoja na Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mohammed Mpinga kujionea hali jinsi ilivyo na kuweza kujifunza mambo mbalimbali katika matumizi ya mradi huo.
"Lengo ni kujifunza matumizi ya njia ili wananchi watambue kuwa njia hii ya mabasi ya kasi haipaswi mtu mwingine kuitumia,tunataka tuone ule umaana wa haraka kutoka kivukoni Kimara.
Waziri mkuu ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na mabasi hayo kuwa yenye usafiri wa uhakika na usio na foleni wala bugudha wanawapa msukumo sasa watumishi wa Umma kuhakikisha kwamba wanapokwenda kazini wananunua tiketi kwa bei nafuu na panda mabasi hayo kwenda kazini na kurudi nayo bila hata ya kuchafuka wanabaki kuwa wasafi tu.
Pia waziri mkuu Majaliwa na Kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani Mohammed Mpinga wameonya madereva wa pikipiki na daladala kuheshimu barabara ya mabasi ya mwendo wa haraka na kuacha kukatiza na kusababisha ajali zisizo na sababu ya msingingi, na kugharimu maisha ya abiria na kuwaacha na ulemavu.
0 comments:
Post a Comment