Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman katika nyanja mbalimbali kwa faida ya nchi zote mbili.
Mheshimiwa Samia ameyasema hayo leo alipokutana na Balozi wa Oman anayemaliza muda wake nchini Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi ambaye alifika ofisini kwake Ikulu kwa ajili ya kumuaga.
"Sisi Tanzania tunajua tuna wajibu wa kukuza uhusiano na Oman, uhusiano wetu siyo wa kibalozi tu, umeota mizizi, kwani ni wa muda mrefu na ni wa kindugu," alisema Makamu wa Rais.
Alibainisha kuwa serikali imekuwa na uhusiano na Oman katika nyanja za elimu na hasa elimu ya juu ambapo Oman imesaidia katika ujenzi wa Chuo cha Afya, Mbweni na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar.
Aidha, alisema serikali ya Oman imeanzisha Mfuko Maalum ikiwa ni ufadhili kwa wanafunzi wa Zanzibar katika elimu ya juu pamoja na kukijengea uwezo Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
Pamoja na misaada hiyo Makamu wa Rais aliiomba serikali ya Oman kuangalia uwezekano wa uwekezaji katika sekta za kilimo na biashara ambako kuna fursa nyingi za uwekezaji.
Katika mazungumzo hayo Balozi Al-ruqaishi alitoa shukrani zake kwa serikali ya Tanzania kutokana na ushirikiano aliopatiwa katika kipindi chote alichokuwepo nchini jambo ambalo limwemwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Home
News
Slider
Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Oman.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment