- Ijumaa iliyopita alifunga bao la kwanza akiwa na timu ya Taifa ya England katika sekundi ya 138 kwenye ushindi wa mabao 2-1
KLABU ya Manchester United inatarajia kutangaza rasmi mkataba mrefu watakaoingia na straika wake Marcus Rashford.
Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa awali.

Mkataba mpya na United atakaosaini anatarajia kulipwa kiasi cha paundi 20,000 kwa wiki.
Rashford amefunga mara mbili katika mechi alizopangwa tangu February kwenye michuano ya Ligi ya Europa waliposhinda dhidi ya Midtjylland FC. Pia alifunga bao lingine katika mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England siku tatu baadaye.
Ndiye mchezaji mdogo kuifungia bao England na anatarajiwa kuwapo katika kikosi cha Roy Hodgson kitakachotajwa kesho Jumanne kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Mataifa ya Ulaya.
Rashford alifunga bao katika sekunde ya 138 kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Australia ikiwa ni mechi yake ya kwanza wakati England iliyokuwa inajiandaa na michuano hiyo itakayofanyika Ufaransa. Mechi hiyo iliyochezwa Ijumaa iliyopita ilikuwa ya kwanza kwa yosso huyo.
Tangu alipoanza kuonyesha kiwango cha juu miezi mitatu iliyopita, Rashford amefunga mabao nane kati ya mechi 18 alizoitumikia klabu hiyo ya Old Trafford.
Katika mazungumzo yanayomhusu kinda huyo, amewakilishwa na ndugu wa familia yake kwa kufuata ushauri wa Chris na Wayne Welbeck, kaka wa straika wa zamani wa United Danny, ambaye sasa anaitumikia Arsenal.
Wakati huo huo United inatajwa kuwa iko katika hatua za mwisho za kumnasa beki Cameron Borthwick-Jackson, ambaye naye mkataba wake umebakiza mwaka mmoja.
Mchezaji huyo mwenye miaka 19 ameichezea timu hiyo mechi 14 ikiwa chini ya Louis van Gaal ambaye alitimuliwa siku mbili baada ya kuipa United ubingwa wa Kombe la FA na nafasi yake tayari imechukuliwa na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho.

0 comments:
Post a Comment