Mshambuliaji wa Yanga Paul Nonga anaripotiwa kwamba, huenda akajiunga na klabu yake ya zamani Mwadui FC baada ya kushindwa kufanya vyema akiwa na Yanga kutokana na nafasi finyu anayoipata kwenye klabu hiyo.
Kupitia segment ya Hili Game ya kipindi cha Powe Breakfast kutoka Clouds FM, nimezinasa tetesi za usajili kutoka katika vilabu kadhaa vya VPL.
Baada ya jana taarifa kusambaa kwamba mshambuliaji wa Yanga Paul Nonga ameuandikia barua uongozi wa klabu yake akitaka kuuzwa kwenye klabu nyingine ili kutnusuru kipaji chake baada ya kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Yanga kutokana na upinzani mkali alioupata kutoka washambuliaji Amis Tambwe, Donald Ngoma, Malimi Busungu na Matheo Anthony.
Inadaiwa kwamba, Nongo ameomba kurejea kwenye klabu yake ya zamani ambapo ya Mwadui FC ya Shinyanga ambapo ndiko Yanga walikomtoa na kumsajili katika kipindi cha dirisha dogo la usajili. Tangu Nonga amejiunga na Yanga, hajapata nafasi ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga kutokana na kocha wa timu hiyo kuwatumia washambuliaji Donald Ngoma na Amis Tambwe huku Malimi Busungu na Matheo Anthony wakiwa chagu mbadala wakati Nonga akipata nafasi finyu.
Jana mtandao huu ulimnukuu Nonga akithibisha kupeleka barua kwenye uongozi wa Yanga akiomba kuuzwa baada ya kushindwa kupambana ndani ya klabu hiyo kupata nafasi ya kucheza.
”Nimeomba kuuzwa na tayari barua ipo mezani kwenye ofisi ya Yanga na nimewatajia mahali ninapopenda kuuzwa, nimeomba kuuzwa ili wasiingie hasara kwasababu walininunua kwa pesa nyingi. Sababu kubwa ya maamuzi Yangu haya ni nafasi finyu ya kucheza niliyonayo katika kikosi cha Yanga kutokana ubora walionao wenzangu wanaocheza nafasi niichezayo na wanatimiza majukumu yao ipasavyo na kuitendea haki nafasi hiyo”, alisema Nonga wakati alifazungumza na Yahaya Mohamedy.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment