Mkali
wa Ligi Ndogo, Bill Nas ameachana na management yake ya zamani Rada
Entertainment ambayo inamilikiwa na TID na kujiunga na label mpya itwayo
‘LFLG.
Bill Nas amesema yeye na Rada kwa sasa wamebaki kama washikaji.
“Rada
sijaondoka ila mkataka wangu mimi na Rada uliisha kwa sababu ulikuwa wa
mwaka mmoja, tena uliisha muda mrefu toka mwaka jana mwezi wa 12. Kwa
hiyo kwa sasa nipo kama familia tu na TID mimi ni kaka yangu, ni mtu
ambaye ana mchango mkubwa kwenye sanaa yangu, kwa hiyo always tupo
pamoja, lakini kibiashara nipo ndani ya label ya ‘LFLG’, hii ndio label
ambayo nafanya nayo kazi, hata Chafu Pozi, audio na video nimeziandaa
nikiwa kwenye label mpya,” alisema Nas.
Rapa huyo ambaye anafanya
vizuri na wimbo wake wa Chafu Pozi, amesema ana inaimani atafanya vizuri
zaidi ndani ya label hiyo mpya kutokana na ushirikiano uliyopo ndani ya
label hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment