Serikali imesema kamwe haitamvumilia askari yeyote Yule wa JWTZ anayefanya vitendo vya unyanyasaji wa raia na itaendelea kuwachukulia hatua kadri wanapobainika .
Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Dr.Husein Mwinyi amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya kuulizwa hatua anazochukua kwa askari ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya unyanyasaji kwa raia.
Dr.Mwinyi amewataka wabunge kuwafichua askari wa JWTZ ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo vinavyolidhalilisha jeshi hilo ili kulinda hadhi na heshima ya jeshi hilo.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi amewasilisha bajeti ya wizara yake leo, nakuomba Bunge liidhinishe Sh1.73trn; matumizi Sh1.48trn, maendeleo Sh248bn.
Pia amesema kuwa serikali imedhamiria kulifanya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania kuwa la kisasa na kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili askari wake.
Home
News
Slider
Serikali kuwachukuluia hatua baadhi ya askari wa JWTZ wanaofanya unyanyasaji kwa raia.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment