Upasuaji huo ni mkubwa wa kwanza na wa aina yake kufanyika hapa nchini na kwa kanda Afrika ya Mashariki na Kati .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam , Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dk. Peter Kisenge amesema wataalam wa taasisi hizo mbili kwa mara ya tatu wameweza kutoa tiba kubwa ya moyo bila mgonjwa kupasuliwa kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa kuzibua Valvu zilizoziba( BMV Procedure ).
Wataalam hao wa Moyo ambao watakuwa hapa nchini kwa siku mbili watatoa mafunzo kwa watoa huduma wa Taasisi ya moyo ambapo wagonjwa watakaopewa huduma hii watafikia takribani 18 .
“ Taasisi itaokoa zaidi ya Shilingi Milioni 180 kwa siku mbili kama wagonjwa hawa wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu haya haya , na kubwa zaidi si fedha tu bali tumeokoa maisha ya watanzania wenzetu” amesema Dk. Kisenge.
Katika hatua nyingine, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imetia saini mkataba wa ushirikiano wa kutoa huduma na mafunzo na Taasisi ya BKL ya nchini India , lengo ni kuwapa mafunzo watumishi wake na kuendelea kutoa huduma ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na taasisi ya BLK .
Kwa mwaka huu peke yake JKCI imefanya procedure 471 ikiwemo upasuaji wa Moyo kwa kufungua kifua 99, vipandikizi 78 , vizibua njia 265 na nyinginezo 29 .
Mbali na ushirikiano huu na Taasisi ya BLK , JKCI imeweza kufanikisha huduma hizi kubwa kwa kushirikiana na taasisi nyingine marafiki zikiwemo Al-Muntada ( Saudi Arabia ) Open Heart International ( Australia) , Save a Child’s Heart ( Israel) na Madaktari Afrika.
Kambi kama hizi zitaendelea tena Julai, Septemba na Novemba .
0 comments:
Post a Comment