Image
Image

UHABA WA SUKARI:Serikali yaingiza tani za Sukari Karibu Elifu 12 nchini.

Wakati suala la uhaba wa sukari nchini likiendelea kuitikisa nchi kila upande hatimaye Serikali imeingiza nchini tani 11,957 za Sukari na zimeshaanza kusambazwa katika kanda zote.
Waziri Mkuu amesema kuwa ifikapofika ijumaa Serikali itaingiza tani elfu 20 ambazo zitasambazwa katika kanda hizo kukabiliana na upungufu Uliopo wa Sukari.
Hata hivyo waziri mkuu Kassim Majaliwa ameagiza sukari inayokamatwa katika Maghala isambazwe Sokoni na kuuzwa kwa bei elekezi ya shilingi 1800 kwa kilo.
Aidha waziri mkuu Majaliwa amekiri kuwa kuna upungufu wa tani laki moja za sukari nchini kutokana na viwanda vingi kutozalisha sukari katika kipindi hiki,huku wengine wakificha sukari hiyo kwenye Maghala.
SAKATA LA SUKARI:
Katika hatua nyingine tumearifiwa kuwa kuna Mfanyabiashara Dar amekamatwa akituhumiwa kuficha sukari tani 4 Kinondoni na hivyo tayari kiongozi wa mtaa ameshatiwa mbaroni akidaiwa kuhongwa afiche siri.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment