Baadhi ya wakulima wa viazi katika ya wilaya ya SIHA mkoani KILIMANJARO wameanza kutekeleza agizo la Serikali la kuacha kufungasha mazao ikiwemo viazi kwa mtindo wa rumbesa.
Wakulima hao wa kata ya NGARENAIROBI wamesema kitendo cha serikali kuzuia rumbesa kimeleta tija kwa wakulima kwani walikuwa wakipata hasara kwa kuwa gunia moja la Rumbesa liliweza kutoa magunia mawili ya mazao.
Kwa upande wake Afisa vipimo Mkuu katika ofisi ya wakala wa Vipimo mkoani Kilimanjaro EPHRAIM ASSENGA amesema licha ya wakulima hao kutumia vipimo halali bado wanaongeza madebe zaidi ya sita ambayo ni zaidi ya kilo mia moja.
Naye Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro SAID MECKY SADICK akizungumza baada ya kutembelea mradi wa umwagiliaji wa MSARIKIE wilaya ya MOSHI amewataka wakulima hao kuacha tabia hiyo ambayo inamnufaisha mnunuzi badala ya kuwanufaisha wakulima.
Home
News
Slider
Agizo la Serikali kwa wakulima kuacha kufungasha Rumbesa kwenye Viazi laanza kutekelezwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment