Kundi la kijihadi la al-Shabaab limeshambulia kituo cha jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia, na kuwauwa kiasi ya wanajeshi 30 wa Ethiopia. Maafisa walisema wanamgambo hao waliripua bomu lililokuwa katika gari katika lango la kituo hicho katika jimbo la Hiran, kabla ya kujaribu kukivamia. Watu walioshuhudia waliripoti kusikia mripuko mkubwa uliofuatiwa na mapigano ya risasi muda mfupi kabla ya alfajiri. Milio ya risasi iliendelea kusikika kwa takriban saa moja baada ya mripuko kusikika. Pande hizo mbili zimetoa taarifa zinazokinzana juu ya
mapigano hayo. Maafisa wa Ethiopia wanadai kwamba shambulio hilo lilizuiwa na kwamba wanajeshi wao wamewauwa zaidi ya wanamgambo 100 wa al-Shabaab. Kundi hilo la al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaeda, limedai kwamba limepoteza wapiganaji 16.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment