Image
Image

Albino:Hatujaridhishwa na mikakati ya kuhakikisha kwamba tupo salama.

WATU wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO), wamesema hawajaridhishwa na mikakati ya kuhakikisha kundi hilo linabaki salama kwenye jamii dhidi ya wauaji na wale wanaowakata viungo vyao.
Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania, (TAS), Musa Katambi, aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa akizungumzia kuhusu Siku ya Kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino itakayofanyika kimataifa Jumatatu ijayo.
Maadhimisho hayo kitaifa ni ya 11 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006 na kimataifa ni ya pili tangu Baraza la Umoja wa Mataifa kuitangaza rasmi Juni 13 ya kila mwaka.
Katambi alisema licha ya juhudi mbalimbali za kukabiliana na watu wanaosababisha vifo na wengine kuwaacha na ulemavu, hawajaridhishwa na kwamba ipo mikakati ya mpasuko.
Kuhusu maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa chama hicho, Nemes Temba, alisema yatafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia Jumamosi hadi Jumatatu ijayo.
Alisema mgeni rasmi wa kilele cha maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa ni Rais John Magufuli.
“Siku ya Jumamosi kutakuwa na mdahalo maalum ambapo waalikwa wenye sifa na taaluma, watashiriki kujadili mada zinazolenga kutafuta suluhu za changamoto zinazotukabili, mdahalo umedhaminiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na utafanyika kwenye ukumbi wao,” alisema.
Pia alisema watoto wenye ualbino wanaoishi kwenye vituo mbalimbali nchini watapata fursa ya kutembelea Bagamoyo kwa ajili ya kujifunza na kupata faraja.
Kuhusu changamoto, Temba alizitaja ni vituo vinavyowalea watoto na vingine vikiwa na vijana, wanawake na wanaume, ni lini amani itarejea kwenye jamii ili warudi kuishi kwa ujumuishi.
“Vituo hivi vilianzishwa kama dharura na siyo makazi ya kudumu, je; ni lini itakuwa mwisho wa vituo hivi?” Alihoji.
Changamoto nyingine ni watoto hao ambao wapo vituoni baadhi yao haijulikani wazazi wake waliko na maeneo walikotolewa.
Imeandikwa na Romana Mallya na Hanifa Ramadhani
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment