Image
Image

Baraza la usalama la umoja wa mataifa kujadili kuhusu misaada SYRIA.

Serikali ya SYRIA imeruhusu Umoja wa Mataifa pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu kuingiza misaada ya kiutu nchini humo mwezi huu.
Miongoni mwa maeneo yaliyoidhinishwa ni 15 kati ya 19 yaliyozingirwa pamoja na maeneo mengine 25. Umoja wa Mataifa umesema helikopta zitatumiwa kupeleka misaada katika maeneo hayo yaliyozingirwa.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana leo hii kujadili mpango wa kutuma misaada kwa njia za angani. 
Wakati huohuo muungano wa kijeshi unaongozwa na Marekani pia umewatumia silaha waasi kwa njia za anga, wanaopigana na kundi la kigaidi la IS wakiwa wanajaribu kulizuia kuingia katika mji wa MAREA.
Aidha mjini ALEPPO, raia 23 wameuawa kutokana na mashambulizi ya serikali, wakati watu wengine wawili wamuawa katika mji wa LATAKIA, baada za mtu mmoja kujiripua kwa bomu.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment