Bidhaa za maziwa nchini Kenya zimeathirika na maziwa ya bei ya chini kutoka Afrika kusini na ulaya,na kuwakosesha wasindikaji wa ndani soko la kuuzia maziwa yao nje ya nchi.
Mwenyekiti wa chama cha wasindikaji maziwa nchini Kenya Nixon Sigey amesema gharama za juu za uzalishaji nchini Kenya zimefanya maziwa ya Kenya kutoweza kushindana katika soko la nje.
Utafiti wa hivi juzi uliofanywa na Taasisi ya Tegemeo umeonesha kuwa gharama za uzalishaji kwa wstani nchini Kenya ni shilingi 16 ilhali utafiti mwengine uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mifugo inasema gharama za uzalishaji ni shilingi 18 kwa kila lita moja.Gharama za Uganda ni shilingi 10 kwa kila lita.
Sigey amesema bidhaa za Kenya zinashindwa kushindana na nchi za Tanzania na Uganda kwa sababu bidhaa za maziwa ziko bei nafuu katika nchi hizo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment