Saa 24 kabla ya kura ya maoni itakayoamua kama Waingereza wasalie au la katika Umoja wa Ulaya, Waziri Mkuu David Cameron anasema hawezi kuashiria matokeo yatakuwa ya aina gani. Hakuna anayejua kutatokea nini, ameliambia gazeti la "Financial Times". David Cameron amesisitiza kwa vyovyote vile ataendelea kuwa waziri mkuu na hajuti kwamba yeye ndiye aliyeitisha kura hiyo ya maoni. Wakati huo huo, viongozi wa karibu nusu ya makampuni makubwa makubwa ya Uingereza wamewataka wakaazi wa nchi hiyo waunge mkono fikra ya nchi yao kuendelea kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Takriban viongozi 1,300 wakiwemo 51 wa makampuni 100 yanayowakilishwa katika soko la hisa la mjini London wameandika risala iliyochapishwa na gazeti la The Times wakisema kujitoa katika Umoja wa Ulaya kutailetea Uingereza madhara makubwa ya kiuchumi. Utafiti wa maoni ya umma unaonyesha matokeo ya kura ya maoni yatakuwa "ya kubanana".
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment