Waziri
wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametangaza
azma ya nchi yake kuwania tena kiti katika Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa kama mwanachama asiye wa kudumu, kuanzia mwaka 2019 hadi
2020.
Steinmeier aliitangaza azma hizo jana mjini Hamburg, katika
hotuba juu ya sera ya uhusiano wa kimataifa. Kwa muda mrefu Ujerumani
imetetea mabadiliko katika Baraza la Usalama, ikitaka kupata kiti cha
kudumu. Kwa mara ya mwisho Ujerumani ilikuwa mwanachama wa Baraza hilo
kati ya mwaka 2011 na 2012.
Kabla ya kura ya kuamua wanachama
itakayopigwa mwaka 2018, Ujerumani itaendesha kampeni kuvutia uungwaji
mkono wa nchi nyingine. Ombi la Ujerumani litahitaji ridhaa ya angalau
theluthi mbili ya wanachama wote 193 wa Umoja wa Mataifa kuweza
kufanikiwa.
Ujerumani, kwa ushirikiano na India, Brazil na Japan,
zinataka mabadiliko makubwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa, ambalo nchi hizo zinasema limepitwa na wakati.
Home
Kimataifa
Frank-Walter atangaza azma ya nchi yake kuwania kiti katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment