Image
Image

Gauck:Nchini Ujerumani Demokrasia haiko hatarini.

Rais Joachim Gauck wa Ujerumani amesema taasisi madhubuti na mashirika ya kijamii yatasaidia kuilinda demokrasia dhidi ya kubadili fikra za umma kuegemea sera kali za mrengo wa kulia.Gauck amelaani mashambulizi yanayofanywa na wafuasi wa sera kali za mrengo wa kulia dhidi ya wakimbizi. Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha taifa ARD Gauck amesema licha ya mtizamo hasi wa wafuasi wa sera kali za mrengo wa kulia dhidi ya wageni na kuongezeka kwa  mashambulizi kwa makaazi ya watafuta hifadhi nchini Ujerumani demokrasia haiko hatarini.Amesema hivi sasa wana taasisi zinazofanya kazi, katiba nzuri,walezi wa demokrasia na jamii madhubuti ya kiraia mambo ambayo hawakuwa nayo hapo kabla. Katika mazungumzo yake hayo hapo jana Gauck pia amepuuzilia mbali ulinganisho wowote ule na siasa zinazoyumba na zilizogawika za kabla ya vita vikuu vya kwanza vya dunia kwa Ujerumani wakati huo ikijulikana kama Jamhuri ya Wieimar.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment