Image
Image

JWTZ kupambana na ugaidi kwa kushirikiana na majeshi ya Afrika mashariki na SADC.

Jeshi la wananchi waTanzania JWTZ limeahidi kushirikiana na majeshi mengine ya ulizi na usalama ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na zile za jumuiya ya kusini mwa Afrika  (SADC) katika kulinda na kudhibiti vitendo vya kigaidi katika nchi hizo.
Mkuu wa chuo cha ukamanda na unadhimu kilichopo Duluti jijini Arusha,Brigedia Jenerali Sylvester Minja amesema hayo wakati akizungumza na ITV ambapo amesema wanatambua vitendo vya kigaidi vinavyoendelea katika nchi nyingi za Kiafrika hali inayosababisha kutokea kwa vitendo vingi vya uvunjifu wa amani.
Amesema kutokana na sababu hiyo ndio maana wanaunganisha nguvu na majeshi katika nchi nyingine za kiafrika sambamba kuwa na mafunzo ya pamoja kimkakati ili kupata ujuzi,nidhamu na maarifa sawa ya kupambana na uhalifu kwani hali ya kiusalama inabadilika kila mara huku mkuu wa wilaya  ya Arusha Fadhili Nkurlu  akibainisha serikali kuunga mkono jiihtihada hizo.
BONYEZ
A HAPA>>http://bit.ly/28TwWIV
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment