Kenya imeungana na nchi nyingine duniani jumapili kuadhimisha siku ya kimataifa dhidi ya madawa ya kulevya.
Siku hiyo inayoadhimishwa kila tarehe 26 Juni hulenga kuhamasisha kuhusu matatizo ambayo madawa ya kulevya yanaleta katika jamii.
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa lankupambana na madawa na uhalifu (UNODC) ,watu milioni 200 duniani wanatumia madawa ya kulevya kama vile cocaine,bangi,heroine n.k.
Akizungumza katika sherehe za siku ya kimataifa ya kupambana na madawa ya kulevya iliyoadhimishwa katika viwanja vya mtaa wa Huruma,waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery amesema serikali iko katika harakati za kushinda vita dhidi ya pombe haramu na madawa ya kulevya katika pwani ya Kenya.
Home
Afya
Slider
Kenya imeungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa dhidi ya madawa za kulevya
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment