Lowassa aikosoa Ripoti ya Jumuiya ya Ulaya kuhusiana na Uchaguzi Mkuu 2015
Aliyekuwa Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe.Edward Lowasa ameikosoa Ripoti ya Jumuiya ya Ulaya kuhusiana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kuwa ilikuwa na dosari nyingi na imetengenezwa katika mazingira ya kukifurahisha chama tawala.
Mhe.Lowasa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani amesema Ripoti hiyo ya Jumuiya ya ulaya ilitakiwa iende mbele zaidi na kuelezea kile kilichofanyika nchini kama kilikuwa ni huru na haki kwa mustakabali wa Demokrasia nchini ambapo pia ameikosoa vikali Tume ya Uchaguzi.
Katika hotuba yake kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ambao ni wanachama wa CHADEMA ,Mhe.Lowasa amesema na kila ushahidi kuwa alishinda Uchaguzi Mkuu katika kiti cha urais mwaka jana lakini ameamua kuwa kimya juu ya hilo kwa mustakabali wanchi.
Baadhi ya wanafunzi hao wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu wamemweleza kuwa walikabiliana na wakati mgumu kipindi cha masomo yao hasa baada ya kuweka wazi hisia zao za kuunga mkono upinzani.
0 comments:
Post a Comment