Image
Image

Mahakama kuu kanda ya Iringa kutoa hukumu ya Mwangosi 21 July,2016.

Mahakama kuu kanda ya Iringa imetaja siku ya tarehe 21 July 2016 kuwa itatoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari mkoani Iringa Daudi Mwangosi inayomkabili askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia ghasia mjini Iringa Pasificus Cleophace Simon.
Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania anayesikiliza kesi hiyo Mheshimawa Dokta Paul Kihwelo ametaja tarehe hiyo baada ya kufanya majumuisho ya kesi na kusikiliza maoni ya wazee wa baraza na baadaye kuitaja tarehe 21 mwezi july kuwa ndiyo siku ya mahakama kutoa hukumu ya kesi hiyo.
Awali akitoa majumuisho ya kesi hiyo jaji Dokta Kihwelo aliwataka wazee hao wa baraza kutotumia kielelezo namba 1 ambacho ni picha ya gazeti la mwananchi toleo la tarehe 3 Septemba mwaka 2012 lililochapisha picha ya askari wa jeshi la polisi wakiwa wameuzunguka mwili wa marehemu mwangosi huku mmoja wao akiwa amemwelekezea bunduki marehemu akisema kuwa kielelezo hicho hakijakidhi vigezo vya kimahakama kwakuwa upande wa jamhuri haukumleta mahakamani mpiga picha wa picha hiyo kutoa ushahidi.
Katika maoni ya mmoja wa wazee wa baraza mahakamani hapo amesema haoni hatia kwa mtuhumiwa kwakuwa shahidi namba moja kamanda wa kikosi cha FFU mjini Iringa Said Mnunka ambaye ndiye aliyeongoza operesheni hiyo alieleza mahakamani jinsi alivyawapanga askari wake lakini yeye mwenyewe akiwa katika eneo la tukio hakumshuhudia mtuhumiwa akimuua marehemu Mwangosi.
Aidha katika maoni ya mzee mwingine wa baraza mahakamani hapo ameeleza kuwa ushahidi wa mmoja wa mashahidi wa upande wa jamhuri ambaye ndiye aliyetoa silaha na kuzipokea baada ya operesheni Lewis Teikya aliieleza mahakama alivyotoa silaha hizo lakini hakueleza kama kulikuwa na upungufu wa silaha wakati wa kuzirejesha huku mmoja wa wazee hao wa mahakama akisema kuwa ushahidi wa ungamo la mtuhumiwa kwa mlinzi wa amani siku tatu baada ya tukio unamtia hatiani mshitakiwa kwakuwa alionesha kukiri kumuua marehemu kwa kueleza kuwa anajutia kufanya kitendo hicho.
 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment