WAKATI Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, akitarajia kusoma bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli inayokadiriwa kufikia Sh. trilioni 30 leo,
Serikali inatarajiwa kuja na vyanzo vipya vya mapato ambavyo huenda vikaongeza ukali wa maisha kuanzia Julai mosi, mwaka huu.
Serikali ya Rais Magufuli imepania kukuza uchumi wa nchi kwa kufyeka sehemu kubwa ya fedha za matumizi za wizara na kuzielekeza kwenye miradi ya maendeleleo na kuonya watumishi waliozoea maisha ya safari za mara kwa mara na kulipwa posho wasahau mambo hayo.
Akizungumza wakati wa shughuli ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara za Nyerere na Tazara jijini Dar es Salaam uliofanyika Aprili 16, mwaka huu, Rais Magufuli alisema serikali itapandisha fedha za maendeleo ili ifikie asilimia 40 kwenye bajeti hii tofauti na bajeti ya mwaka wa fedha 2015/16, ambapo fedha za maendeleo zilikuwa asilimia 26 tu.
“Tunataka hizi fedha za chai, semina, na posho zote zikatwe na zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo. Ili zifanye kazi kwenye afya, elimu, barabara na ununuzi wa ndege,” alikaririwa Rais Magufuli wakati huo.
Ili kufikia lengo la bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 ambayo inakabiliwa changamoto ya baadhi ya wahisani kujitoa, serikali inatarajiwa kuongeza vyanzo vya mapato tofauti na vile vilivyozoeleka kama soda, sigara, bia, pombe kali, kodi za mishahara na tozo mbalimbali kwenye nishati ya mafuta ya magari na yale ya taa.
Baadhi ya maeneo ambayo kwa sasa yanatarajiwa kuguswa na serikali ni pamoja na kuongeza kodi mbalimbali kwenye simu (vocha na miamala), kodi ya majengo, maeneo ya kumbi za starehe na kubana wafanyabiashara wadogo na hasa wenye kipato cha kuanzia Sh. Milioni 15 kwa mwezi.
Pia inatarajiwa kuongeza kodi kwenye bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na magari na pia kufuta misamaha mbalimbali ya kodi na hasa ile inayotolewa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na kampuni mbalimbali zilizowekeza nchini.
Serikali pia inaweza kuangalia vyanzo vya mapato vilivyoainishwa kwenye ripoti ya Kamati ya Bajeti ya Bunge la 10, iliyokuwa inaongozwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki (CCM), Andrew Chenge maarufu kama `Chenge One’.
Baadhi ya vyanzo vya mapato vilivyokuwa kwenye ripoti hiyo ni pamoja na uvuvi wa bahari kuu, kupiga mnada vitalu vya misitu na vya uwindaji wa kitalii, kupiga mnada masafa ya mawasiliano na kodi za majengo.
Wakati wa Bunge lililopita Chenge alikaririwa akisema;“Tukiangalia uvuvi wa Bahari Kuu, kamati inashangazwa na sababu inayotolewa na Serikali kwamba haiwezi kukusanya mapato hayo hadi hapo itakapojenga bandari maalum ya uvuvi (fish port) wakati inapoteza takribani Dola za Marekani milioni 222 sawa na Sh bilioni 372,960 kwenye sekta hiyo.
Hali ilivyo Akiwasilisha mwelekeo wa ukomo wa bajeti ya mwaka 2016/17, Aprili 6, mwaka huu, Dk. Mpango alisema katika bajeti hiyo ya Sh trilioni 29, mapato ya ndani yanatarajia kuwa Sh. trilioni 17.79 na kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajiwa kukusanya Sh. trilioni 15.1.
Alisema makusanyo yasiyo ya kodi yanatarajiwa kuwa Sh. trilioni 2.69 huku makusanyo ya halmashauri zote yakiwa Sh. bilioni 665.41 na kwamba serikali inatarajia kupata Sh. trilioni 3.6, ikiwa ni misaada ya wahisani kwenye bajeti kuu ya serikali na miradi mbalimbali wanayoifadhili moja kwa moja.
Kadhalika, serikali inatarajia kukopa mikopo ya masharti ya kibiashara Sh. trilioni 2.1 kutoka vyanzo vya nje na Sh. trilioni 5.37 kutoka vyanzo vya ndani.
Mwaka wa fedha wa 2015/16, Serikali ilitarajiwa kukusanya jumla ya Sh trilioni 13.8, hivyo ndani ya mwaka mmoja wa fedha, utawala wa Rais Magufuli unataka kukusanya Sh trilioni 4.7 zaidi.
Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 25. Ili kukidhi pengo hilo, Serikali haina budi kuongeza kodi kwa kiwango cha asilimia 25 ili kuweza kutimiza malengo yake ya makusanyo.
Taarifa kutoka serikali zinadai, Serikali imepanga kuchukua kodi zote za majengo ili kuongeza makusanyo yake. Kwa upande wa simu za mikononi, ambapo kwa sasa ni takribani watu milioni 28 wanatumia simu, kodi inatarajiwa kuongezwa kwenye kupiga simu na katika miamala ya kutoa ama kutuma fedha.
Kwa upande wa kubana wafanyabishara wadogo, serikali inatarajiwa kusambaza mashine za kutoa risti za TRA, kwa wafanyabiashara ambao kwa mwezi wanafanya biashara ya Sh milioni 15.
Hali hiyo pia inaelezwa kwamba itaongeza makusanyo ya serikali ambapo kwa sasa wafanyabiashara wengi wanakwepa kodi.
Pia uagizaji wa bidhaa kutoa nje ya nchi ni eneo jingine ambalo linaaminika litabanwa ili kuongeza mapato huku watakaoumia zaidi wakiwa ni wale wanaoagiza magari yaliyotumika.
Kwa Tanzania watu wengi huagiza magari yenye mpaka miaka 20, huku sheria ya kodi ya uchakavu ikiwa inaanza kubana wale wanaoagiza magari yenye kuanzia umri wa miaka nane.
Chanzo kingine cha mapato ambacho kuna taarifa kinaweza kuguswa ni kile cha kumbi za starehe na harusi ambapo kwa mwezi hufanya biashara ya mamilioni ya fedha lakini hakuna kodi inayotozwa.
Misamaha ya kodi ni eneo jingine ambalo litafanya serikali kuokoa mamilioni ambapo asasi za kiraia na zile za dini zinazonufaika na misamaha mbalimbali ya kodi zinatarajiwa kubanwa.
Pia kampuni mbalimbali zikiwamo za madini zinatarajia kubanwa kwenye kodi. Kwa mujibu wa ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali (CAG), misamaha ya kodi inayotolewa kwa kampuni za uchimbaji wa madini pekee kwa mwaka 2011, ilikuwa Sh bilioni 109,885 huku misamaha iliyotolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), ikifikia Sh bilioni 239.667.
Pia kumekuwepo na malalamiko kwamba, baadhi ya misamaha inayotolewa kwenye asasi za kiraia na taasisi za dini hutumika vibaya, ambapo kwa sasa kuna shinikizo zinapaswa kumulikwa.
Bajeti ya mwaka 2015/16, ilikuwa ya Sh trilioni 22.5, na ilijikita zaidi kufanikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, huku ile ya mwaka 2014/15 ilikuwa Sh. trilioni 19.85 na mwaka 2013/14 ilikuwa Sh. trilioni 18.2.
Bajeti hiyo inakuja wakati ambapo baadhi ya wahisani wametangaza kukata misaada yao kwenye bajeti ya Tanzania, huku wengine wakiondoa fedha zao kwenye miradi mbalimbali waliyokuwa wakiifadhili kutokana na kutoridhishwa na uchaguzi wa Zanzibar.
Kwenye bajeti ya serikali ya 2014/15 wahisani walitarajiwa kuchangia Sh. trilioni 1.09, lakini wengi walikataa kutoa fedha kutokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.
Marekani imeshatangaza kuifuta Tanzania kwenye nchi wanachama wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), hivyo nchi kukosa Sh. trilioni 1.03 ilizokuwa ipewe na shirika hilo kusaidia ujenzi wa barabara za pembezoni na kusambaza umeme vijijini.
Hata hivyo, nchi hiyo imetoa imeahidi msaada wa kiasi cha Sh. Trilioni 1.7, ambazo zitatolewa nje ya MCC. Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress alitoa ahadi hiyo wakati alipokutana na Rais Magufuli juzi jijini Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment