Akijibu
Maswali ya Wabunge Mjini Dodoma, katika kipindi cha maswali na
majibu,Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Charles Mwijage amesema kila wilaya
ianzishe mitaa ya viwanda ili kuwasaidia wakulima kunufaika na mazao yao
kwa kudhibiti udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara kwa kuwanyonya
wakulima.
Mhe. Mwijage amesema kuwa atalazimika kununua mizani pamoja
na mashine za EFDS na kuweka vituo vya mauzo hayo ili kuleta tija kwa
wakulima huku akiongeza kwa kusema kuwa sasa kutakuwa na kipimo maalumu
cha uzito wa kufunga mizigo yao.
Kwa upande mwingine,akizungumzia
viwanda vilivyobinafsishwa, Mhe.Mwijage amesema wawekezaji wote
waliopewa viwanda na wameshindwa kuviendeleza serikali inawataka
wavirudishe mara moja.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment