Image
Image

Mzambia kuanza na TP Mazembe, Tambwe nje

KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm ameagiza straika mpya, Obrey Chirwa pamoja na Juma Abdul waende haraka Uturuki kujiunga na kambi tayari kwa mechi ya TP Mazembe itakayopigwa Jumanne ijayo Dar es Salaam.

Kama mchezaji huyo atafanikiwa kwenda leo au kesho Uturuki inamaanisha atakuwa na wiki moja tu ya kujiweka sawa mazoezi kwa kuvisoma vyenga vya Ngoma na mafowadi wengine kabla ya kukabidhiwa kijiti cha Tambwe ambaye atakuwa shabiki jukwaani.

Yanga baada ya kumsainisha ilianza kwa kuwasilisha haraka jina lake Caf na kitu pekee ambacho kinaweza kuwa kikwazo kwake kucheza ni kama klabu yake ya FC Platinum itatoa zuio lolote, ingawa Yanga wamesisitiza wameshamalizana nao kiroho safi.

Tambwe ana kadi mbili za njano, ambazo zitamfanya akose mechi ijayo dhidi ya TP Mazembe Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm ameiambia Mwanaspoti mjini hapa kwamba, ameagiza Chirwa na Abdul waje haraka kwavile hakuna namna.

Pluijm alisema Chirwa ni muhimu kwenye kikosi chake na tayari usajili wake umeshawahishwa Caf ili kuangalia uwezekano wa kumchezesha dhidi ya Mazembe.

“Tambwe ana kadi, Oscar Joshua ameumia na yule Haji Mwinyi ameonyeshwa nyekundu hivyo, lazima tufanye mbadala wa haraka,”alisema Pluijm.

Kocha huyo ana imani kwamba mchezaji huyo anaweza kuwa sawa ndani ya muda mfupi kwavile ametoka kwenye Ligi ya Zimbabwe na aliwahi kucheza na Donald Ngoma kwenye klabu ya FC Platinum na ana uzoefu wa kutosha kwenye mechi za kimataifa.

Abdul ambaye alikuwa majeruhi akaachwa Dar es Salaam ameitwa ili kuangalia uwezekano wa kuziba nafasi ya Oscar na Mwinyi ambao hawatacheza mechi ijayo.

Pluijm alisisitiza kwamba mechi ijayo ni ya kufa kupona na lazima watulize mpira chini washinde maneno ambayo yameungwa mkono na winga, Simon Msuva.

Yanga iliondoka Bejaia jana Jumatatu jioni kurejea kambini mjini Antalya, Uturuki ambapo itakwea pipa kuja Dar es Salaam juni 27 siku moja kabla ya mchezo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment