Jaji Francis Mutungi amekutana na watumishi kutoka ofisi yake na kupata nafasi ya kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi ya kila siku ikiwa ni moja ya shughuli katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma. Pichani akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano wa watumishi.
Katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma yenye kauli mbiu“uongozi wa umma kwa ukuaji jumuishi: kuelekea katika afrika tunayoitaka” Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mhe. Jaji Francis S. K Mutungi jana amekutana na watumishi kutoka ofisi yake na kupata nafasi ya kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika kutekeleza majukumu yao ya kikazi ya kila siku.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo uliopo kivukoni Ilala, Mtaa wa Shabani Robert jijini Dar es salaam.
Akitoa majibu ya baadhi ya changamoto hizo, Jaji Mutungi aliwashukuru watumishi wote kwa kazi nzuri ya kulijenga taifa na amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uaminifu, ueledi na kwa bidii zaidi ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.
“Serikali ina dhamira nzuri katika kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo tunapaswa kuhakikisha kwamba dhamira ya Serikali inatekelezwa kwa vitendo” alisisitiza Jaji Mutungi
Kwa upande wao watumishi wameiomba Serikali kuona namna nzuri ya kushughulikia changamoto mbali mbali za watumishi .
Siku hiyo maalumu ya kusikiliza changamoto na maoni ya watumishi ni utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa agizo la Serikali katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa Umma iliyoanza Juni 16-23, 2016.
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa pia imetenga siku ya kesho Ijumaa ya tarehe 24 Juni, 2016 kwa ajili ya kukutana na wadau wake kwa lengo la kutoa elimu na kupokea changamoto wanazokumbana nazo wadau hususani katika masuala yanayohusu Vyama vya Siasa na sheria zake .
Home
News
Slider
OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment