Image
Image

Rais wa Burundi atoa siku 15 kwa makundi yenye silaha kujisalimisha kwa vikosi vya usalama.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ametoa siku 15 kwa makundi yenye silaha katika mikoa ya Bururi na Rumonge kujisalimisha kwa vikosi vya usalama.
Akihutumia wananchi katika wilaya ya Mugamba, ambayo imeshuhudia vurugu nyingi kutoka kwa makundi yenye silaha katika siku za karibuni, rais Nkurunziza amesema baada ya siku hizo kumalizika, vikosi vya usalama vitapambana na makundi hayo bila huruma. Amesema mikakati na mbinu za kuyamaliza makundi yenye silaha mjini Bujumbura itatumika katika wilaya ya Mugamba mkoani Bururi na katika maeneo ya mkoa wa Rumonge.
Rais Nkurunziza amesisitiza kuwa, uchaguzi uliofanyika mwaka jana umemalizika na hauwezi kufanyika tena, na kwamba sasa ni wakati wa kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2020, mwaka 2025,na miaka mingine.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment