Leo ni siku ya wakimbizi duniani ambapo taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inasema idadi ya wakimbizi na watu waliopotezewa maakazi yao imevunja rekodi kwa kufikia watu milioni 65.3 hapo mwaka 2015.
Katika ripoti iliyotolewa leo hii na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kati ya kila kundi la watu 113 duniani aidha linakuwa linapotezewa makaazi ndani ya nchi zao,wakimbizi au watafuta hifadhi.Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu hao wanalazimika kukimbia makaazi yao kutokana na vurugu za matumizi ya nguvu,ukandamizaji na mizozo na hii ni mara ya kwanza kwa idadi hiyo kuvuka milioni 60. Ujerumani imepokea maombi mengi ya watafuta hifadhi kuliko nchi nyengine yoyote ile duniani hapo mwaka 2015.
Home
Kimataifa
Slider
SIKU YA WAKIMBIZI:Wakimbizi na watu waliopotezewa maakazi yao ni Milioni 65.3, Mwaka 2015.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment