Image
Image

Sudan yavitaka vyama mbalimbali ya upinzani kusaini mapema makubaliano ya mpango wa amani.

Msaidizi wa rais wa Sudan ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Chama tawala cha nchi hiyo NCP Bw. Ibrahim Mahmoud Hamid, amesema serikali inavitaka vyama mbalimbali vya upinzani visaini mapema makubaliano ya mpango wa amani, na kukutana baada ya sikukuu ya Eid.
Bw. Hamid amesema makubaliano hayo yaliyotolewa na Umoja wa Afrika ni fursa ya kukomesha vita ya ndani na kufikisha misaada ya kibinadamu kwenye sehemu zilizoathirika.
Kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu mashambulizi yamekuwa yakitokea kwenye sehemu mbalimbali za Darfur. Wiki iliyopita gavana wa jimbo la Darfur Kaskazini Bw. Abdul Wahid Yusuf alitangaza kuwa, vikosi vyote vya usalama viko kwenye tahadhari ya hali ya juu, ili kukabiliana na vurugu zinazoendelea katika jimbo hilo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment