Image
Image

Syria yalaani vikosi vya kigeni kuingia nchini humo bila ruhusa


Wizara ya mambo ya nje ya Syria imetoa taarifa ikilaani vikali vikosi maalumu vya kigeni kuingia kaskazini nchini humo bila kupata ruhusa ya serikali.
Taarifa imesema hivi karibuni kuna ripoti kuhusu kuingia kwa vikosi vya Ufaransa na Ujerumani katika sehemu za Ayn al Arab na Mambij, kitendo ambacho ni kinyume na katiba ya Umoja wa Mataifa na uchokozi dhidi ya mamlaka ya Syria, na kusisitiza kuwa operesheni halali ni lazima ziungwe mkono na serikali ya nchi hiyo.
Hata hivyo wizara ya ulinzi ya Ujerumani imekanusha habari kuwa imetuma vikosi maalumu nchini humo, na habari kutoka serikali ya Ufaransa zinasema kikosi chake maalumu kinasaidia makundi ya upinzani ya Syria kupambana na kundi la IS.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment