Image
Image

TANZIA‬,Muhammad Ali afariki dunia.

Bingwa wa zamani wa Dunia wa ngumi za uzani wa juu (World Heavyweight Champion) anayeaminika kuwa mmoja kati ya Mabondia bora zaidi kuwahi kutokea Ulimwenguni, Muhammad Ali almaarufu kama "The Greatest" amefariki Dunia katika hospitali ya Phoenix-area iliyopo Phoenix, Arizona alipokuwa amelazwa kwa matibabu. 
Ali ambaye ni Bingwa mara tatu wa ngumi za Uzani wa Juu amefariki dunia akiwa na umri wa Miaka 74.
Muhammad Ali aliyestaafu ndondi za kulipwa mwaka 1981 aligundulika kuwa na ugojwa wa Parkinson (Parkinsons Disease) Mwaka 1984 na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo hadi alipopatwa na mauti siku ya Ijumaa. Mbali na ugonjwa huo pia Ali alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi pamoja na maambukizi katika njia ya mkojo.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment