Matibabu hayo ambayo kwa kawaida hufanyika katika nchi za India, Afrika Kusini, Ulaya na Marekani, yameendeshwa kwa siku mbili na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Taasisi hiyo ambayo inauda sehemu ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hatua yake imeifanya isvunje rekodi ya kimataifa.
Upasuaji huo na nyingine zinazoendelea katika taasisi hiyo, ni matokeo chanya ya serikali ya kuimarisha JKCI katika vifaa na wataalamu wenye uwezo mkubwa.
Wiki iliyopita walishuhudiwa wataalamu wageni wanaofika kujifunza, ili kuongeza ujuzi na kubadilisha uzoefu.
Mei 23 mwaka huu, madaktari bingwa wa moyo wa JKCI walishirikiana na wenzao kutoka hospitali ya BLK ya India, walifanikiwa kuokoa maisha ya Watanzania waliokuwa na matatizo ya moyo, bila ya kupanda ndege kwenda kutafuta huduma hiyo nje.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo, Bashir Nyangaza, anasema hivi sasa hawahitaji wagonjwa wa moyo waende nje ya nchi, kwa sababu wana uwezo mkubwa kwa kufanya kazi hiyo nchini.
“Tumejidhatiti kufanya mambo makubwa zaidi. Lengo letu ni kuokoa pato la taifa, upo upasuaji ambao moyo na mapafu lazima uisimamishwe na damu hiyo huwekwa kwenye mashine maalum (heart lung machine) ambayo ndio inayofanya kazi,” anasema Dk. Nyangasa:
“Upasuaji huu tuliofanya, moyo wa mgonjwa unaendelea kufanya kazi kama kawaida. Tunachofanya ni kuvuna mishipa ya damu kwenye miguu, kisha unaipandikiza katika moyo,” anaeleza.
Dk. Nyangasa anafafanua namna wanavyofanya kazi ni kwamba, wanakifungua kifua halafu wanakutana na moyo na ndipo wanapoweza kufanya upasuaji wa kutumia mashine au vinginevyo.
“Upasuaji bila kutumia mashine unafanyika kwa kuvuna mishipa ya damu kutoka miguuni na kuileta kwenye moyo na tunaangalia pale palipoziba, kwa kuifanya mishipa hiyo kama daraja,” anasema.
“Unaweza kukuta mtu mmoja anakuwa na vipande vitano vya mishipa ya damu ya moyo vilivyoziba, hivyo unavuna mishipa ya miguuni na kupeleka damu sehemu zote za moyo,” anasema
Dk. Nyangasa anasema upasuaji wa aina hiyohufanyika kwa wagonjwa wenye tatizo la moyo wenye tundu na hata kwa watoto.
Anasema upasuaji huo unapunguza muda na bei yake haitofautiani na ule wa kutumia mashine na anongeza: “Kati ya upasuaji wa kutumia mashine na huu bila mashine, ulio salama zaidi ni wa bila mashine.
“Ni kwa sababu kutumia mashine, ile damu inayopita kwenye mashine, husagwa sagwa na mgonjwa anaweza kuingia kwenye upasuaji na damu 90 na anatoka na damu 70.”
TOFAUTI YA GHARAMA
Mkuu wa Kitengo cha Matibabu ya Moyo, Dk. Peter Kisenge, anasema gharama ya kumpelekea mgonjwa nje huwa hufikia Sh. milioni 25, lakini kwa kufanya nchini ni Sh. milioni 10 ambayo ni nafuu kwa asilimia 60, kwa maana gharama ya nchini ni asilimia 40 ya ile inayofanyika nje ya nchi.
Dk. Kisenge anasisitiza kuwa, mgonjwa anayetumia mashine, hahitaji gharama na upasuaji unapofanyika, mgonjwa huchukua muda mrefu kutoka Chumba Maalum cha Wagonjwa Mahututi (ICU), wakati wa bila mashine anatoka haraka.
Mtaalamu huyo anaongeza kuwa, upasuaji bila mashine hutumia uniti ndogo za damu (tatu), wakati kwa mashine huhitajika damu uniti 90, zinazowekwa kwenye mashine.
Anasema hiyo ni changamoto kutokana na uhaba wake wa kila mara.
Kuhusu wataalam kutoka India walioshirikiana nao kwenye upasuaji huo bila ya kutumia mashine, Dk. Kisenge anasema takriban wagonjwa 18 ndio waliokuwa katika orodha ya kufanyiwa upasuaji huo.
“Upasuaji huu ni mkubwa na kwanza na wa aina yake kufanyika hapa Tanzania na kwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
“Tumeweza kutoa tiba kubwa ya moyo bila mgonjwa kupasuliwa kwa kutumia mtambo wa ‘Cathlab’ kwa kuzibua valvu zilizoziba,” anabainisha.
Anasema, ili kuimarisha ushirikiano, JKCI na BLK zimetia saini hati maalum ya ushirikiano ambayo Dk. Kisenge anaeleza ni kwa ajili ya mafunzo ya watumishi wanaotoa huduma ya upasuaji.
Katika utiaji saini hiyo, Dk. Kisenge anasema, wataalam hao watakuwepo kwenye taasisi hiyo kwa siku mbili kutoa mafunzo kwa watoa huduma wa taasisi yake ya Jakaya Kikwete.
Anafafanua kuwa, mbali na upasuaji wa wagonjwa 18, wameweza kuokoa Sh. milioni 180 kwa siku mbili, kama serikali ingewapeleka nje ya nchi kwa matibabu hayo.
“Na kubwa zaidi sio fedha tu bali tumeokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuendeleza kutoa huduma hii,” anasema.
Dk. Kisenge anasema kwa mwaka huu pekee JKCI imefanya operesheni 471 ikiwemo upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua (99), vipandikizi (78), kuzibua njia (265) na nyinginezo (29).
Mbali ya ushirikiano wa BLK, mtaalamu huyo anasema kuwa taasisi hiyo imefanikisha huduma hizo kwa kushirikiana na taasisi nyingine anazozitaka kuwa ni: Al-Muntada ya Saudi Arabia, Open Heart International ya Australia na Save a Child’s Heart ya Israel na Madaktari Afrika.
UJIO WA MADAKTARI
Pia anasema kambi kama hizo za madaktari kutoka nje zitaendelea kuwapo tena mwezi Julai na Septemba, wakitarajiwa kupokea wataalam kutoka Marekani.
Dk. Kisenga anasema mwezi Novemba watakuwa mna madaktari kutoka Israeli, Ujerumani na Austraria.
Mwenyekiti wa BLK, Dk. Ajay Kaul, anasema wameamua kusaidia, kwa sababu tatizo la moyo barani Afrika ni kubwa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi, anataja baadhi ya vyanzo vya matatizo ya moyo, kwamba ni mfumo wa maisha ya kila siku ya mwanadamu, ikiwamo vyakula anavyotumia na msongo wa mawazo.

0 comments:
Post a Comment