Image
Image

Uamuzi kesi vigogo Rahco Juni 13.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepanga kutoa uamuzi Juni 13, mwaka huu kuhusu uhalali wa kushtakiwa vigogo watatu wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (Rahco), akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Benhardard Tito.
Tito na wenzake wanakabiliwa na kesi ya kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Dola za Kimarekani 527,540.
Mbali na Tito washtakiwa wengine ni, mfanyabiashara Kanji Mwinyijuma na Katibu wa Rahco, Emmanuel Massawe.
Akiahirisha kesi hiyo jana, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alisema mahakama yake itatoa uamuzi huo Juni 13, mwaka huu.
Awali wakili wa utetezi Jerome Msemwa aliwasilisha vielelezo ikiwamo barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuhusu uhalali wa kumshtakiwa Kanji kwa madai kuwa tuhuma zilizopo mahakamani hazina ushahidi dhidi yake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment