Image
Image

Valls:Abballa alikula kiapo cha utii kwa kundi la Dola la Kiislamu

Waziri  mkuu  wa  Ufaransa Manuel Valls  amesema  leo kwamba  nchi  hiyo  inafanya  kila  inaloweza  kuzuwia mashambulizi  ya  kigaidi  lakini  yatakuwapo  mengi.
Aliyasema  hayo  kufuatia kile  maafisa  nchini  Ufaransa walichosema  kwamba mtu  aliyefanya  shambulio  baya  la mauaji  ya  watu  wawili  alikula  kiapo  cha  utii kwa  kundi la  kigaidi  la  Dola  la  Kiislamu.
Larossi Abballa  mwenye  umri  wa  miaka  25 alimchoma kisu afisa  wa  polisi  hadi  kufa   katika  kitongoji  cha  jiji  la Paris  usiku  wa  Jumatatu, kabla  ya  kumuua  mke  wa afisa  huyo  nyumbani  kwao. Abballa  binafsi  aliuwawa baadaye  kufuatia  mapambano  ya  masaa  matatu na polisi.
Jana  Jumanne, maafisa  walisema  kwamba  Abballa alikula  kiapo  mara  kadhaa  kwa  kundi  la  Dola  la Kiislamu  na  kiongozi  wake, Abu Bakr al-Baghdadi katika video  ya  dakika  13 aliyoichukua  mwenyewe  nyumbani kwa  wahanga.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment