Image
Image

Wasioielewa Kasi ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu tafadhali wasiturudishe nyuma.

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, juzi na jana alikaririwa na vyombo vya habari nchini akitolea ufafanuzi juu ya kauli ya Rais, John Magufuli ya wanasiasa kuachana na porojo za kisiasa, akiwasihi wasubiri hadi mwaka 2020.
Amesema kiongozi huyo wa nchi hajazuia siasa, bali anachohitaji ni ushirikiano kutoka kwa wanasiasa wenzake ili kuwaletea maendeleo wananchi. Amelazimika kuyasema hayo baada ya wanasiasa wa vyama vya upinzani kuijia juu kauli ya kiongozi huyo wa nchi, wakidai anaminya uhuru wa kujieleza na kurudisha nyuma juhudi zilizopigwa kidemokrasia.
Mara baada ya kupokea Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Alhamisi wiki hii, Rais Magufuli kwa unyenyekevu aliwaomba wanasiasa nchini kuacha siasa kila wakati na kuwataka kutumikia wananchi.
Kauli hiyo ilikuwa sawa na kuwakumbusha wabunge wa upinzani juu ya umuhimu wa kuwatumikia wananchi waliowachagua majimboni, badala ya kila mara kususia vikao vya Bunge na mambo mengine kwa madai kuwa, hawatendewi haki.
Katika siku za hivi karibuni, wabunge wa upinzani wamekuwa na madai kuwa wanabaguliwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson na hivyo kuamua kususia vikao vyote anavyoviongoza, jambo linaloathiri ushiriki wao katika vikao vinavyoendelea vya Bunge la Bajeti kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
Aidha, kutokana na uonevu wanaodai kufanyiwa, na baada ya baadhi yao kutimuliwa bungeni kutokana na utovu wa nidhamu, walikusudia kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara, jambo lililopingwa na Polisi, ikielezwa kilichoonekana ni kama wanataka kuvuruga amani ya nchi kwa kuwachonganisha wananchi na serikali yao, kwani hawakuwa na hoja ya msingi.
Kwa kuona ushiriki wao duni katika kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo, pengine ndiyo maana Rais akazungumzia ubaya wa siasa zisizo na tija na jinsi zinavyowapotezea muda wanasiasa na Watanzania kwa ujumla.
Na katika kuonesha hana dhamira mbaya na wapinzani, Rais alidiriki kusema yuko tayari kushirikiana na wanasiasa hao ili kufanikisha maendeleo ya nchi yao. Ndiyo maana akawasisitiza kuachana na siasa za hivyo, ili wawainue kiuchumi wananchi waliowaamini na kuwapa kura.
Ndivyo alivyokusudia Rais Magufuli, ndivyo walivyoelewa wasomi waliomwagia sifa kauli ya `kuachana’ na siasa, lakini pia ndivyo walivyomwelewa wananchi walio wengi na ndivyo tulivyomwelewa sisi.
Kwamba, siasa za kususa na kuvizia matukio ndiyo wengine waibuke na kuongea, zisipewe uzito kwa kipindi hiki cha mapambano ya kuinua uchumi wa nchi, bali kila mmoja alenge kuisaidia nchi kukua kiuchumi kupitia kaulimbiu ya `Hapa Kazi Tu’.
Wanachotaka kusikia Watanzania kwa sasa ni juu ya ustawi wa nchi, si malumbano na mipasho ya kisiasa inayoendelea hata baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Nasi tunasema, kauli ya Ra
is ilikuwa na maana kubwa mno kwa kuhimiza ustawi wa nchi, tofauti na upotoshaji unaolazimishwa kugeuzwa ukweli kwa lengo la kutafuta umaarufu wa kisiasa. Kwa wakati tulionao, ni vyema tukaungana kuijenga nchi bila ya kujali itikadi za kisiasa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment