Image
Image

Waziri Mkuu Mstaafu Dkt.SALIM AHMED SALIM awataka vijana kujua historia ya nchi.

Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. SALIM AHMED SALIM ametoa wito kwa vijana nchini kujua historia ya nchi na kudumisha ushirikiano na nchi nyingine kwa maendeleo ya taifa na AFRIKA kwa ujumla.
Dkt. SALIM  amesema hayo jijini DSM katika hafla ya kutunukiwa MEDALI YA URAFIKI na serikali ya CUBA, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya nchi hiyo.
Kwa upande wake Balozi wa CUBA hapa nchini JORGE LOPEZ TORMO amesema nchi hiyo inatambua mchango wa Dkt. SALIM kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo CHE GUEVARA.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi na mabalozi  wa nchi mbalimbali,  huku mgeni rasmi akiwa ni Rais wa awamu ya pili  mzee ALI HASSAN MWINYI.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment