11 wafa na wengine kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari 3 Dakawa,Morogoro.
Watu kumi na mmoja wamefariki dunia na wengine wengi wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, katika eneo la VETA, Dakawa, tarafa ya Magole Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.
Magari hayo matatu ni pamoja na lori la kubeba mafuta, lori lililokuwa libeba mchele na vitunguu na basi la abiria mali ya kampuni ya ETA ambalo lilikuwa linatoka Bukoba kwenda Dar es Salaam.
Chanzo cha ajali hiyo ni lori la kubeba mafuta lilikuwa linakwepa lori jingine lililokuwa linalipita lori lori lenye konteina lililobeba mchele, lakini wakati linapita likakutana lori la kubeba mafuta likitokea Morogoro kwenda Dodoma na kusababisha moto kuwaka na watu kupoteza maisha.
Miongozi mwa waliokufa ni mwendesha Bodaboda aliyekuwa akipokea abiria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ULRICH MATEI amesema muda wa basi hilo la abiria lipopita eneo hilo majira ya saakumi alfjiri haliruhusiwi kuendelea na safari kwa mujibu wa sheria.
Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na Kituo cha Afya cha Dumila kwa matibabu zaidi.
0 comments:
Post a Comment