Mahakama
kuu nchini Uganda, imemuachia kwa dhamana kiongozi mkuu wa upinzani na
aliyekuwa mgombea Urais kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Dr. Kizza
Besigye.
Mwanasiasa huyo wa chama cha The Forum for Democratic
Change, FDC, alikuwa anazuiliwa kwenye gereza la Luzira akituhumiwa kwa
kosa la uhaini.
Akitoa uamuzi wake, Jaji Wilson Masalu Musene,
amesema kuwa dhamana anayopewa Besigye ni ishara ya haki ya kisheria ya
mtuhumiwa, ya kwamba hana hatia hadi pale atakapopatikana na hatia au
mtu kukiri kosa.
Jaji Masalu ameongeza kuwa "kipekee Besigye kama watuhumiwa wengine, alikuwa anahudhuria vikao vya kesi yake kwa uaminifu".
Besigye,
mgombea wa nafasi ya Urais kwa zaidi ya mara nne na kushika nafasi ya
pili kwenye chaguzi zote, mwezi February mwaka huu baada tu ya
kumalizika kwa uchaguzi wa rais, alijiapisha ambapo baadae alishtakiwa
kwa kosa la uhaini.
Kwa mujibu wa sheria za Uganda, kifungu namba 23
cha Penal Code, kinasema kuwa, mtu akipatikana na hatia ya kosa la
uhaini, hukumu yake ni adhabu ya kifo.
Makosa mengine yanayomkabili
Besigye ni pamoja na kujitangaza mshindi kinyume cha sheria, kukaidi
amri halali ya polisi na kuitisha maandamano kinyume cha sheria pamoja
na kula kiapo kinyume na sheria za nchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment