Wajumbe
wa chama cha Democratic nchini Marekani wamemuidhinisha Bi Hillary
Clinton kuwa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho katika
uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu. Bi Clinton
anakuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya Marekani kuwa mgombea
urais wa chama kikubwa cha kisiasa nchini humo.
Akizungumza katika
mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika mjini Philadelphia aliyekuwa
mpinzani wake wakati wa kura za mchujo Seneta Bernie Sanders alitangaza
kumuunga mkono Bi Clinton kuwa mgombea rasmi wa chama hicho. Mume wa
Hilary Clinton, Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton naye pia alipata
nafasi ya kutoa hotuba na kumuunga mkono Bi Clinton akisema kwa sasa
ana sifa zinazomuwezesha kuwa rais ajaye wa taifa hilo. Bi Clinton
ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani anatarajiwa
kuchuana na mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi
huo wa Novemba.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment