NYOTA
wa mchezo wa tenisi raia wa nchini Australia, Johanna Konta, ametwaa
ubingwa wa michuano ya WTA baada ya kumshinda bingwa mara saba wa Grand
Slam, Venus Williams.
Venus amejikuta akiwa katika wakati mgumu kwa
mara ya pili, ikiwa ni wiki mbili zilizopita akitolewa kwenye nusu
fainali ya michuano ya Wembledon, huku mdogo wake, Serena Williams,
akitwaa ubingwa huo.
Katika mchezo wa juzi, Konta mwenye umri wa
miaka 25, alifanikiwa kumshinda bingwa huyo mwenye umri wa miaka 36, kwa
seti 7-5 5-7 6-2.
Hata hivyo, mshindi huyo amedai kwamba furaha yake
kubwa ni kuweza kushinda mbele ya bingwa wa mchezo huo, hivyo atakuwa
na furaha ya muda mrefu.
“Furaha yangu ni kufanikiwa kutwaa ubingwa
huu mbele ya nyota wa mchezo huu, najua haikuwa kazi rahisi kushinda
taji hili kwa kuwa mpinzani wangu anajulikana kwa kuwa na uwezo mkubwa.
“Nilikuwa
na wasiwasi mkubwa baada ya kugundua kuwa nitacheza na Venus, lakini
uwezo wangu umenifanya niwe hapa kwa sasa, mpinzani wangu ana uzoefu
mkubwa na ametwaa mataji mengi ila kwa upande wangu ninaamini nimefanya
vizuri zaidi,” alisema Johanna.
Kwa upande wa Venus naye amempa
pongezi mpinzani wake Johanna kwa ushindi huo ambao ameupata na amemtaka
kujituma zaidi ili kuweza kufanya vizuri katika michuano mingine.
“Johanna
alistahili kushinda, alionesha uwezo wa hali ya juu japokuwa nilimpa
changamoto mbalimbali, ninaamini ataendelea kufanya vizuri katika
michuano mingine kutokana na uwezo wake ambao anauonesha.
“Kikubwa
anatakiwa kupambana kwa kufanya mazoezi ya nguvu ili kujihakikishia
anafanya makubwa zaidi katika michuano mingine,” alisema Venus.
Hata
hivyo, mchezaji huyo anadaiwa kufanya vizuri tangu Januari mwaka huu
ambapo aliweza kufika kwenye fainali ya michuano ya wazi ya Australia na
michuano ya Eastbourne, Juni mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment