Maafisa kadha wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya mtu mwenye silaha kushambulia kituo cha polisi eneo la Kapenguria, kaskazini magharibi mwa Kenya.
Mtu
huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru mshukiwa aliyekuwa
amekamatwa akishukiwa kuhusika katika ugaidi, gazeti la Daily Nation
limeripoti.
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano wameuawa.
Mkuu wa polisi wa kituo hicho Vitalis Ochido anadaiwa kujeruhiwa.
Ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.
Tovuti ya habari ya Capital FM imemnukuu mkuu wa polisi Joseph Boinnet akisema polisi zaidi wametumwa eneo hilo.
“Mshukiwa
wa ugaidi aliyekuwa anazuiliwa alitwaa bunduki na kuanza kuvyatua
risasi," Bw Boinnet amenukuliwa. "Kituo hicho sasa kimezingirwa na
juhudi za kukabiliana naye (mshambuliaji) zinaendelea."
Home
Kimataifa
Slider
Kenya kwafukuta:Polisi wahofiwa kufa baada ya Al Shabab kushambulia kituo cha polisi
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment