Rais John pombe Magufuli amewataka Wakurugenzi wa Wilaya,Miji na Majiji kuhakikisha kuwa wanaenda kufanya kazi kwa kushirikiana na Wakuu wa mikoa na kuacha kuwasikiliza watu wenye dhamira ya kuwakwamisha kwa kigezo kuwa hawana Experience ya kutosha kazini.
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati wa Kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri , Manispaa na wilaya, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiongea nao na kuwataka kuachana na historia za experience maana kuna watu wanalalamika kuhusiana na kuteua watu wasio na experience, ambapo ameshangazwa na mitandao ya kijamii kumuandika Luhende kama Msomi mwenye cheti cha hotel Management wakati ana Masters na alikuwa mkaguzi wa elimu wa kanda.
Rais anasema amepitia kwenye mtandao mmoja wa kijamii akaona comment za watu juu ya Luhende akabaki kucheka tu,amemsimamisha Luhende na kuwataka waandishi wa habari wampige picha na waende Sinza kumpiga picha Luhende Meneja wa Hotel na kuzisambaza mitanadaoni
Rais pia anasema anawafahamu Wakurugenzi wake wote,anasikia malalamiko kwenye mitandao ya kijamii,amewaambia wajishangilie wao na si kusikitika kwa kutokushangiliwa na mitandao ya kijamii,anasema hao wasioshangilia kwenye mitandao ni maadui zake,..."Watachonga sana lakini wataka kimya"
Rais anasema zamani nafasi za ukurugenzi zilikuwa "deal",na pale TAMISEMI kulikuwa na mtandao wa kuhongwa ili kuwapatia watu ukurugenzi,aliishagiza Waziri awaondoe wapo watatu pale utumishi ambao kazi yao ilikuwa kuhongwa na kugawa vyeo vya Ukurugenzi.Rais anasema Wakurugenzi wote aliwapitia jina kwa jina na ndio maana hasafiri ili kufanya mambo yeye mwenyewe na wakati mwingine hulala hata saa nane ili kujiridhisha mambo.
Rais amepiga marufuku Wakurugenzi kutoa "tender" kwa Madiwani na Wanasiasa wafanyabiashara ambao hutumia nafasi zao kushinda zabuni,wapinge kodi ndogondogo kwa wananchi kama za kina mama wauza mchicha,ambao halmashauri zinadai kodi wakati hata mbolea wala mbegu hawakuwasaidia.Watumie madaraka ya kisheria kuwaondoa "watumishi" Miungu watu kwenye vijiji,kata,tarafa na wilaya.
Rais anasema hawezi kuchagua mtu ambaye hawezi kutekeleza sera ya chama cha Mapinduzi wala aamini katika Chama cha Mapinduzi sababu wananchi walichaguwa Chama cha Mapinduzi kutokana na uzuri wa ilani yake.Kwenye mitandao ya Kijamii anasikia kuwa watu wanalalamika anachaguaa watu wasio na "experience",anasema yeye hataki mambo ya ma-experience experience tu,hawezi kuchagua mtu mwenye experience wakati ni mwizi.Kuna watu walijipanga na kutuma "vimemo" ili watu wao wachaguliwe kwenye nafasi hizo,akawafutilia mbali wote waliotumwa na waliotuma.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment