Timu
ya Mpira wa Miguu Ufukweni ya Tanzania imepangwa kucheza na Ivory Coast
kati ya Agosti 26, 27 au 28, 2016 kuwania nafasi ya kucheza fainali za
Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 zitakazofanyika Lagos,
Nigeria.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika kati ya Septemba 16, 17, au 18.
Fainali
za Mpira wa Miguu Ufukweni ambazo zitafahamika pia kama 2016 CAF Beach
Soccer Championship, zitafanyika kuanzia Desemba 13 hadi 18, 2016 jijini
Lagos, Nigeria kwa kushirikisha timu nane.
Tayari Nigeria imepasishwa kuwa mshiriki kwa sifa ya uenyeji wake. Timu nyingine 14 zinawania kucheza fainali hizo.
Timu
nyingine zinazowania ni Cape Verde v Senegal, Uganda v Misri, Liberia v
Morocco, Kenya v Ghana, Msumbiji v Madagascar, Sudan v Libya.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment