Image
Image

AU yatangaza kuunga mkono serikali ya Uturuki kwa niaba ya Umoja wa Afrika

Mkuu wa baraza la usalama la AU Ismail Al-Sharkawi ametangaza kuunga mkono serikali ya Uturuki kwa niaba ya Umoja wa Afrika.Al-Sharkawi alitoa maelezo hayo alipohudhuria sherehe za maadhimisho ya sikukuu ya ushindi ya Agosti 30 iliyoandaliwa katika ubalozi wa Uturuki mjini Addis Ababa.
Katika maelezo yake, Al-Sharkawi alisema, ‘‘Sisi kama Umoja wa Afrika tunapinga jaribio la mapinduzi lililoendeshwa mwezi jana na kuunga mkono serikali na wananchi wa Uturuki.’’
Al-Sharkawi alitangaza msimamo huo kwa kuzingatia uamuzi wa kupinga mapinduzi ya aina yoyote uliochukuliwa na Umoja wa Afrika katika mkutano uliofanyika nchini Algeria mwaka 1999.
Al-Sharkawi pia alifahamisha kwamba Uturuki imekuwa na uhusiano mzuri wa kisiasa na mataifa ya Afrika, jambo ambalo linapaswa kuunga mkono kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano.
Wakati huo huo, Al-Sharkawi pia alibainisha furaha yake kwa hatua ya kutia saini makubaliano na Uturuki kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugaidi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment