Mahabusu
aliyekuwa akishikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Arusha
aliyetambulika kwa jina la Victoria Wenga (51) mkazi wa Lemara jijini
Arusha amejinyonga hadi kufa usiku wa kuamkia jana kwa kutumia shuka
lake bila kuacha ujumbe wowote.
Marehemu alikamatwa Agosti 21 mwaka
huu majira ya Alfajiri kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba yake na maduka
yake mawili kutokana na ugomvi wa kifamilia.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Arusha, Charles Mkumbo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika Kituo
cha Kikuu cha Polisi saa 6:20 usiku jana wakati wenzake wakiwa wamelala.
“Polisi
wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa kike
ambapo polisi walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo, lakini
ilishindikanika,” alisema Kamanda Mkumbo.
Mahabusu huyo, ambaye
ni mkazi wa Lemara jijini Arusha, alijinyonga kwa kutumia shuka lake
alilokuwa anatumia kujifunikia wakati yuko mahabusi. Mtuhumiwa huyo,
alijinyonga kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yake.
“Jana ilikuwa afikishwe mahakamani kujibu kosa lililokuwa linamkabili,”
alisema Kamanda Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya usalama kituoni
hapo na tukio hilo, havihusiani na sababu zozote za kiusalama.
Marehemu
Victoria anadaiwa kuwa na ugomvi wa kifamilia na mume wake
aliyetambulika kwa jina la Edward Wenga akimtuhumu kuzaa nje ya ndoa
kinyume na utaratibu.
Imeelezwa kuwa hicho ndo chanzo cha marehemu
kufikia hatua ya kuteketeza mali walizochuma na mume wake ambazo ni
maduka mawili na nyumba ya kuishi.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhia mahiti Hospitali ya Mount Meru.
Home
News
Slider
Mahabusu aliyekuwa akishikiliwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Arusha ajinyonga.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment