JESHI la Polisi Zanzibar limejipanga katika kukabiliana na Operesheni UKUTA kwa kufanya mazoezi makali na kuonya kuwa watu wasithubutu kujitokeza Septemba 1.
Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bwana Mohamed Sheikhe Mohamed wakati wakifanya mazoezi ya kujiweka na utayari na vitendo vya uhalifu kwa vikosi mbalimbali vya jeshi la polisi visiwani Zanzibar.
Mazoei ya kujiweka utayari yamefanyika katika mji wa Cheke chake na mitaa yake yote visiwani humo nakuonya watu watakaojitokeza kuandamana Septemba Mosi mwaka huu wasithubutu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment