BINGWA wa mchezo wa tenisi nchini Marekani, Serena Williams,
anatarajia kuweka rekodi ya 23 katika michuano mikubwa ya Grand Slam
katika US Open.
Nyota huyo alishindwa kushiriki michuano ya Cincinnati wiki iliyopita
kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya bega baada ya kurudi katika
michuano ya Olimpiki nchini Brazil.
Mbali na kusumbuliwa na maumivu hayo, kocha wake, Patrick
Mouratoglou, amedai kuwa nyota huyo bado bega lake alijawa sawa kwa
asilimia 100, lakini anaweza kucheza michuano hii ya US Open na kuweka
historia.
Bingwa huyo namba moja kwa ubora duniani kwa upande wa wanawake,
anatarajia kushuka dimbani leo dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini
Urusi, Ekaterina Makarova, huku kocha huyo akidai kuwa maumivu ya Serena
si makubwa na hayawezi kumsumbua.
“Maumivu ya Serena ndani ya siku hizi chache yametulia, ni wazi
kwamba bega hilo halijakamilika kwa asilimia 100, lakini bado kidogo
sana kupona, hivyo kwa sasa yupo katika hali zuri ya kupambana.
“Alikwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil lakini bega
lilimfanya ashindwe kufanya vizuri, nguvu zake anazimalizia kwenye
michuano hii ya US Open,” alisema Mouratoglou
Serena alifanikiwa kufanya vizuri katika michuano ya Wimbledon mwezi
uliopita na kutwaa taji hilo alipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri
katika michuano ya Olimpiki lakini aliyaaga mashindano hayo mapema.
Tangu atolewe kwenye michuano hiyo ya Olimpiki, hadi sasa
hajafanikiwa kushuka dimbani, lakini leo ataonesha uwezo wake katika US
Open.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment